Kayıtlar

YANGA WAFUNGUKIA ISHU YA KUMCHUKUA LUIS MIQUISSONE

Resim
  UONGOZI wa Yanga umeweka wazi kuwa hakuna kinachoshindikana kuhusu ishu ya nyota wa Simba Luis Miquissone anayetajwa kutua hapo kwa mkopo akitokea Klabu ya Al Ahly ya Misri. Kumekuwa na tetesi kuwa Luis ambaye tayari amewaaga Simba kuwa hatakuwa nao msimu ujao wa 2021/22 huenda akaibuka  ndani ya Yanga kwa mkopo kwa kuwa anatajwa kuuzwa Al Ahly ya Misri ambao wao wemeamua kumtoa kwa mkopo. Kaimu Katibu Mkuu wa Yanga, Haji Mfikirwa amesema kuwa ni suala la mashabiki wa Yanga kusubiri nini kitatokea kwa kuwa muda bado upo kwa sasa na kila kitu kitajulikana siku ya kilele cha Wiki ya Mwananchi,  Agosti 29. "Siku hiyo tutakuwa na sapraizi nyingi sana kwa mashabiki, kuhusu suala la kumchukua Luis kwa mkopo kutoka Al Ahly hakuna kitu kunachoshindikana, hivyo watu waendelee kusubiri wanachotakiwa ni kuhudhuria Tamasha la Wiki ya Mwananchi, ". Bado haijawa rasmi kwamba Luis Miquissone anaweza kujiunga na Al Ahly kwa kuwa uongozi wa Simba ulibainisha kuwa timu iliyomchukua iliomba a

DUH! UNAAMBIWA KIPA MPYA YANGA ANADAKA MPAKA MISHALE

Resim
INJINIA Hers Said, Mjumbe Kamati ya Usajili wa Yanga amesema kuwa kipa ambaye amesajiliwa kutoka nchini Mali, Diarra Djigui anadaka mpaka mishale. Nyota huyo inaelezwa kuwa amepewa dili la miaka miwili alikuwa na timu iliyoweka kambi nchini Morocco kabla ya kusitishwa na sasa timu ipo ndani ya ardhi ya Tanzania. Injinia amesema:"Umeona ile timu ambayo tumesajili. Yule Diarra ni bonge moja ya kipa na anadaka mpaka mishale ukiachana na mpira hivyo ni usajili mzuri ambao tumefanya. "Ukiachana na Diarra una beki Djuma Shaban, una Kibwana Shomari,Dickson Job, Bakari Mwamnyeto unadhani Mukoko, (Tonombe)," amesema. Agosti 29 Yanga inatarajia kuwa ni kilele cha Wiki ya Mwananchi ambapo watatambulisha wachezaji wake wapya pamoja na benchi la ufundi.

VIDEO; KOCHA SIMBA ANAAMINI WATAJENGA UFALME KWENYE SOKA LA VIJANA

Resim
KOCHA wa timu ya vijana ndani ya Simba, Mussa Mgosi amesema kuwa wachezaji aliokuwa anawatafuta katika mchujo tayari amepata timu kamili jambo ambalo linampa nafasi ya kuweza kutengeneza timu nzuri.  Mgosi anaamini kwamba atatengeneza wachezaji wazuri watakaokuja kufanya mambo makubwa katika ardhi ya Tanzania na wanaweza kupandishwa kwenye timu kubwa kama ilivyokuwa kwa Ibrahim Ajibu, Jonas Mkude.   

SAKATA LA MORRISON NA YANGA NGOMA BADO MBICHI

Resim
  MAHAKAMA ya usuluhishi ya masuala ya kimichezo CAS bado haijaweza kutoa maamuzi yoyote yale kuhusu kesi ya mchezaji wa Simba kwa sasa Bernard Morrison maarufu kama mzee wa kuchetua. Bado ngoma ni mbichi kwa kuwa muda wowote ule hukumu hiyo inaweza kutolewa. Kwa mujibu wa CAS kesi hiyo ilitarajiwa kutolewa hukumu siku ya Agosti 24 ila mpaka kufikia majira ya saa sita usiku ngoma ilikuwa haijaeleweka bado. Klabu ya Yanga ilipeleka shauri lake kwenye mahakama hiyo wakimlalamikia Morrison kuweza kusaini dili jipya ndani a Simba ilihali alikuwa na mkataba wa miaka miwili ndani ya kikosi hicho. Kwa upande wa mchezaji mwenyewe alikuwa anabainisha kwamba alisaini dili la miezi sita ndani ya Yanga na muda wake uliisha hivyo alisaini dili jipya akiwa ni mchezaji huru. Kwa mujibu wa Kaimu Katibu wa Yanga, Haji Mfikirwa alisema kuwa nao pia walikuwa wanasubiri majibu kutoka Cas ila hawakuyapata jambo ambalo linawafanya waendelee kusubiri. "Matarajio yetu ilikuwa ni kuona kwamba tunapata mre

LWANDAMINA: TUNAREJESHA UTIMAMU WA WACHEZAJI

Resim
  GEORGE Lwandamina,  Kocha Mkuu wa Azam FC amesema kuwa wachezaji wake walikuwa wanafanya mazoezi ya utimamu wa mwili katika mchezo wa kirafiki dhidi Red Arrows.  Kwenye mchezo huo wa kurejesha utimamu wa mwili Azam FC ilipoteza kwa kufungwa mabao 4-0 huku Lwandamina akiweka wazi kuwa kuna jambo ameliona kwa wachezaji wake. "Nilikuwa nataka kuona wachezaji wanarejea katika utimamu wa mwili hasa kutokana na uchovu pamoja na kukaa muda mrefu bila kucheza mechi za ushindani. "Hata namna wachezaji walicheza bado walionekana hawajawa tayari hivyo taratibu wanarejea katika hali ya kawaida ni jambo la kusubiri," amesema.  Azam FC imeweka kambi nchini Zambia kwa ajili ya maandalizi ya msimu mpya wa 2021/22 na itawakilisha Tanzania katika mashindano ya kimataifa ikiwa ipo kwenye Kombe la Shirikisho.

REAL MADRID WABISHI, WAWEKA MKWANJA WA MAANA KUIPATA SAINI YA MBAPPE

Resim
KLABU ya Real Madrid bado haijakata tamaa kuhusu kuipata saini ya mshambuliaji wa PSG, Kylian Mbappe kwa kuamua kuwasilisha bonge moja ya ofa. Sasa Real Madrid inayoshiriki La Liga imeamua kuwasilisha kiasi cha pauni milioni 137 ambayo ni sawa na bilioni 434.8 kwa fedha ya Tanzania. Imeelezwa kuwa Rais wa Real Madrid, Florentino Perez ameweka kiasi hicho cha fedha mezani ili kuhakikisha wanampata mshambuliaji huyo kabla ya dirisha la usajili kufungwa. Mbappe amekataa kusaini mkataba mpya ndani ya PSG na unatarajiwa kumeguka Juni 30 mwakani na usajili wa Ulaya unatarajiwa kufungwa Agosti 31.

SIMULIZI YA MUME ALIYEKUWA AKIPIGWA NA MKEWE KILA WAKATI

Resim
SIMULIZI ya mume aliyekuwa akipigwa na mkewe kila wakati. Ama kwa hakika ndoa hua rahisi kwa mtu ambaye hajawahi ingia kwenye ndoa. Kwa ufahamu wangu  suala zima la ndoa ni ngumu sana haswa ukipata mpenzi asiyekuelewa kwa vyovyote vile ama aliye na  kazi nzuri kuliko wewe kama mume.  Mapenzi huwa na mambo mbalimbali ambayo watu wengi huwa  hawazungumzii kwa undani kwa kuogopa kuchekwa na marafiki wao wa karibu wao husahau kwamba  wanapozungumza msaada unaweza kuja kwa wakati wowote. Kati yao nilikuwa mwadhirika.  Niliishi na  mke wangu Cate kwa furaha hadi wakati ambapo alianza kuninyoosha kwa makonde nisijue hata pa  kukimbilia kila usiku. Alikuwa ni mwanamke  ambaye mwili ulikuwa umemkubali ajabu. Alikuwa ni Polisi na mimi nilikuwa ni dalali wa kuuza maji mjini Kakamega. Marafiki zangu  walinikataza wakati mmoja kwamba mwanamke yule angeniangusha lakini yote yalipata sikio la kufa. Mapenzi yalikuwa yamenoga na hakuna chochote nilikuwa nasikia isipokuwa Cate. Kila mara alipotoka kazin